Share news tips with us here at Hivisasa

Maafisa wa kuzima moto katika Kaunti ya Kisii wamelahumiwa vikali kwa kutowajibikia kazi yao vilivyo kwa muda unaofaa.

Hii ni baada ya ya maafisa hao kuchelewa kufika katika shule ya upili ya wasichana ya Bishop Mogendi Nyakegogi iliyochomeka siku ya Jumatatu asubuhi na kupelekea hasara kubwa ambapo bweni la wanafunzi 25 wa kidato cha nne liliteketea.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu katika shule hiyo, kasisi wa kanisa ya kikatholiki ya Nyamagwa Christopher Oira aliwakosoa maafisa wa kuzima moto wa kaunti kwa kuchelewa kufika shuleni humo ili kuzima moto huo, jambo ambalo lilipelekea bidhaa vya wanafunzi kutookolewa.

“Hawa maafisa wa kuzimo moto wa kaunti yetu ya Kisii hawawajibikii kazi yao vilivyo, maana walipigiwa simu na wakakawia kufika, na walipofika walipata tayari bidhaa vya wanafunzi vimeungua,” alisema Oira.

“Naomba maafisa hao wawe wanawajibikia kazi yao kama wanahitaji kutoa msaada wa kuzima moto ili kuokoa mali yanachomeka kupitia mikasa ya moto,” aliongeza Oira.

Aidha, afisa anayesimamia mikasa katika Kaunti ya Kisii Patrick Lumumba alikanusha madai hayo na kusema walipopigiwa simu waliweza kuwajibika kwa muda uliofaa.

“Tulifika kwa muda na tukazima moto ingawa tulipata bidhaa vingine tayari vilikuwa vimeungua," alisema Lumumba.