Mabwenyenye nchini wameonywa dhidi ya kuuza ardhi za serikali.
Akizungumza siku ya Jumatano katika mkutano na wakazi wa Likoni baada ya mzozo wa ardhi tata ya Waitiki kukamilika, na harakati ya kuandikisha wakazi hao kuanza, mwenyekiti wa Tume ya Ardhi nchini NLC Mohamed Swazuri, alisema kuwa watakaopatikana wakiuza ardhi hizo ambazo ziko chini ya usimamizi wa serikali watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha, Swazuri amewataka wakazi kutoa habari kwa idara husika pindi tu wanaponyanyaswa wakiwa katika ardhi zao.
Haya yanajiri baada ya kushuhudiwa kuuzwa kwa ardhi za serikali kinyume cha sheria hasa katika eneo la Pwani.
Vile vile, Swazuri amewataka wakazi kukoma kuuza ardhi zao kiholela kwa kusema kuwa hatua hiyo itapunguza idadi ya maskwota nchini.