Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Madaktari wa hospitali ya Nyamira level five wamewaokoa wanafunzi wawili wa shule ya upili ya Tabaka iliyoko eneo bunge la Mugirango Kusini baada ya kunywa sumu kwa kutaka  kujitoa uhai.

Hii ni baada ya wanafunzi hao kufumaniwa na mwalimu mmoja wa shule hiyo wakiwa na simu shuleni, jambo ambalo ni kinyume na sheria za shule hiyo, na baada ya kufukuzwa nyumbani kuwaleta wazazi wao, waligopa kuenda nyumbani ndiposa wakaamua kujiua. 

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne, daktari mkuu wa hospitali ya Nyamira Cyrus Ayunga alisema waendeshaji bodaboda wa eneo la Nyabite waliwafumania wasichana hao wamekunywa sumu hiyo barabarani na kuwakimbiza katika hospitali hiyo na kuokolewa .

Ayunga alisema wanafunzi hao walihudumiwa baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo na afya yao inaendelea kuwa shwari, huku akisema wanafunzi hao walikuwa tayari wameandika notisi ya kujitoa uhai baada ya kufukuzwa shuleni.

“Wanafunzi hawa walikuwa watatu lakini wawili ndio walikunywa sumu, lakini tumewahudumia na wanaendelea kupata nafuu,” alisema Ayunga.

“Tulifumaniwa tukiwa na simu shuleni tukatumwa wazazi tukaogopa ndio tukaamua kununua sumu ili tujitoe uhai ,” alisema mmoja wa wanafunzi hao

Wazazi wamewalaumu walimu kwa kuwafukuza wanafunzi nyumbani badala ya kuwaita wazazi ili kusuluhisha kosa linapotokea.