Share news tips with us here at Hivisasa

Wahudumu wa magari ya uchukuzi mjini Mombasa sasa wanaitaka mamlaka ya uchukuzi na usalama barabarani NTSA kuwapa siku zaidi ili waweze kuzifuata sheria mpya za uchukuzi zilizowekwa na mamlaka hiyo wiki iliyopita.

Jame Owino ambaye ni mmoja wa madereva mjini humo, anadai kuwa siku walizopewa na NTSA ni chache mno hivyo wengine wao hawengeweza kuyafanyia magari yao mabadiliko ili kuambatana na sheria hizo mpya.

Akizungumza na mwandishi huyu mapema Jumatatu mjini Mombasa, Owino, aidha amewalaumu maafisa wa NTSA wanaokagua magari barabarani kwa kile amekitaja kama unyanyasaji kutokana kwa maafisa hao.

Owino vilevile ameitaka mamlaka hiyo kuangazia upya sheria inayowataka madereva kua na miaka 25 na zaidi kwani ameitaja kama inayowakandamiza wengine wenye uwezo wa kuyaendesha magari japo wana umri mdogo.

Kauli ya dereva huyo inajiri wakati mamlaka ya uchukuzi na usalama barabarani NTSA ikianzisha msako siku ya Jumatatu kuyaondoa magari yasiofuata sheria mpya za barabara.

Msako huo umechangia wenye magari kuongeza nauli na kusababisha malalamishi kutoka kwa abiria.