Maafisa wa polisi mjini Mombasa wamelifunga bohari moja katika eneo la Changamwe baada ya kunasa maelfu ya magunia ya mchele na nafaka nyingine zenye thamani ya mamilioni ya fedha zinazoaminika kupitwa na wakati wake wa matumizi.
Siku ya Jumatano, Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa alisema kuwa maafisa hao wamenasa magunia hayo ya mchele yaliongizwa humu nchini kutoka milki za Kiarabu na mchele huo ulikuwa ukipakiwa upya katika mifuko mingine kuuzwa.
Marwa aliwakashifu maafisa wa Halmashauri ya ulipaji ushuru nchini KRA akidai maafisa wa halmashauri hiyo pamoja na baadhi ya maafisa wa polisi wanashirikiana na mabwenyenye kuingiza bidhaa gushi humu nchini pamoja na kukwepa ulipaji ushuru.
Mafisa wakuu wawili wa bohari hilo wamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi.
Amehoji njia zilizotumika kuingiza bidhaa hizo humu nchini licha ya kupitwa na wakati akitaka shirika la kukadiri ubora wa bidhaa nchini KEBs na KRA kuwajibika.