Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Magavana wote nchini wameombwa kupunguza ziara nyingi na kutumia pesa hizo kuleta maendeleo katika kaunti zao.

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa magavana nchini huwa na ziara nyingi na kutumia pesa nyingi kwa safari huku nyingine za safari hizo hazina umuhimu wowote.

Akiongea siku ya Jumapili katika eneo bunge lake la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira, mbunge wa eneo hilo Timothy Bosire aliomba magavana kupunguza ziara za safari na kutumia pesa hizo za ziara nyingi kuleta maendeleo katika kaunti zao ili kwanufaisha wananchi.

“Wananchi wanastahili kupokea maendeleo kutoka kwa magavana katika kaunti zao lakini mara nyingi magavana huwa na ziara nyingi za safari na kutumia pesa nyingi ambazo zingefanya maendeleo,” alisema Bosire.

“Naomba ziara hizo zipunguzwe ili pesa zile zitumike kuleta maendeleo kwa wananchi haswa kukarabati barabara, kuanzisha miradi ya maji na miradi mingine ya maendeleo ambayo ni ya kunufaisha wakazi,” aliongeza Bosire.

Aidha, Bosire alilalamika kwa kudai kuwa ufisadi unaendelea kukithiri mizizi katika serikali za kaunti huku akiomba ufisadi kupunguzwa katika serikali hizo.

“Ufisadi ndio umeongezeka katika serikali za kaunti na kuchangia kurudi nyuma kwa maendeleo naomba ufisadi ukomeshwa ili sisis sote viongozi tuungane kuleta maendeleo ufisadi ni jambo mbaya ambayo huumiza wakazi wengine na kuleta umaskini,” aliongeza Bosire.