Share news tips with us here at Hivisasa

Magenge ya kihalifu yanayowasumbua wakazi wa Kisauni mjini Mombasa hasa lile la ‘Wakali kwanza’ na ‘Wakali wao’ yameonya vikali kusalimu amri ya maafisa wa polisi la sivyo yakabiliwe kikamilifu.

Akitoa onyo hilo, Kamanda mkuu wa polisi eneo la Pwani Francis Wanjohi alisema kuwa magenge hayo yamewahangaisha wakazi kwa muda mrefu na lazima yakabiliwe kisheria ili wakazi kuishi kwa amani.

Kwenye mahojiano na mwanahabari huyu mjini Mombasa siku ya Jumanne, Wanjohi alisema kuwa iwapo watakaidi agizo la maafisa hao na kuanza kukabiliana nao, basi maafisa wa polisi watatekeleza jukumu lao kikamilifu kulingana na mafunzo ya kiusalama waliyopewa na serikali.

"Tunayashauri magenge ya kihalifu kusalimu amri na kuachana na uhalifu kabla ya maafisa wetu wa polisi kuvamia maficho yao,” alisema Wanjohi.

Wakati uo huo, wamewatahadharisha viongozi wa kisiasa wanaoyafadhili magenge ya kihalifu katika eneo zima la Pwani kuwa watatiwa nguvuni na kuwaonya kutowagonganisha wakenya.