Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama ya Mombasa imeipa polisi makataa ya siku 15 kumchunguza kijana mmoja mwenye umri wa miaka 24, anayehusishwa na ugaidi.

Mshukiwa huyo kwa jina Ikrima Mohamed Soshi anahusishwa na kundi la Al-Shabaab.

Akitoa agizo hilo baada ya afisa wa upelelezi Peter Munguti kuambia mahakama kuwa mshukiwa anahifadhi washukiwa wa ugaidi nyumbani kwake, hakimu Nicholas Njagi alisema siku ya Ijumaa kuwa uchunguzi uwasilishwe mara moja ili kuthibitisha madai hayo.

Shosi alikamatwa katika mkahawa mmoja ya burudani mjini Mombasa, na anahusishwa visa kadhaa vya uhalifu na ugaidi.

Kesi yake itatajwa tena katika mahakama hiyo ya Mombasa baada ya uchunguzi kukamilika.