Mahakama kuu ya Naivasha ndio itaskiza kesi ya mauaji ya mwanamziki wa nyimbo za kikalenjin Diana Chemutai maarufu kama Chelele. Aliyekuwa bwanake Eric Musila ndiye anakabiliwa na mashataka ya mauaji ya Chelele. Mahakama kuu ya Kericho ilihamisha kesi hiyo hadi mahakama ya Naivasha siku ya Jumatatu.
Hapo awali, kesi hiyo ilikosa kuendelea katika mahakama hiyo ya Kericho baada ya mashahidi kukosa kufika.
Pia wakaazi na wafuasi wa mwanamziki huyo wamekuwa wakijaa mahakama ya Kericho kufuatilia kesi hiyo.
Chelele alipatika ameuawa Nyumbani kwake Kapkwen kaunti ya Bomet.
Mshukiwa huyo wa mauaji anatarajia kuanza kujibu mashtaka kwenye mahakama hiyo ya Naivasha kuanzia Februari 9.