Share news tips with us here at Hivisasa

Makahaba 26 waliotiwa mbaroni mjini Kisii wameagizwa kupimwa ugonjwa wa ukwimwi kwa siku tatu sijazo ili kujua hali zao.

Agizo hilo lilitolewa na jaji wa mahakama ya Kisii John Njoroge baada ya makahaba hao kufikishwa mbele ya mahakama hiyo mnamo siku ya Jumatatu na kusomewa mashtaka ya kukataa kupimwa ugonjwa wa ukimwi walipotiwa mbaroni kufanya ukahaba wakiwa walevi, kutojua hali zao miongoni mwa mengine.

Mnamo siku ya Ijumaa wiki jana, makahaba 300 walitiwa mbaroni mjini Kisii na kulazimika kupimwa ugonjwa huo, huku hao 26 waliokataa na kuwekwa rumande hadi walipofikishwa mbele ya mahakama hiyo siku ya Jumanne na kusomewa mashtaka yao.

Wakili wa makahaba hao Ogutu Mboya aliiambia mahakama kuwa ni kukiuka haki za kibinadamu wanapowalazimisha makahaba kupimwa ugonjwa wa ukimwi kabla ya kuitia ombi hilo wao wenyewe.

Aidha, alikosoa maafisa wa polisi kuwatia mbaroni makahaba na kuwaweka rumande tangu siku ya Ijumaa hadi Jumatatu walipofikishwa mahakamani kabla ya kujua ni lipi walikosa na kuwekwa rumande

Hata hivyo, malalamishi ya wakili huyo yalionekana kutokuwa na msingi wowote huku makahaba wakiagizwa kupimwa ugonjwa huo kwa siku tatu zijazo.

Makahaba hao walikanusha makosa hayo waliosomewa na kuachiliwa kwa faini ya shillingi 2,000 kila mmoja, huku kesi hiyo kuagizwa na jaji Njoroge kusikizwa tarehe thelathini mwezi huu.