Share news tips with us here at Hivisasa

Wanaharakati wa maswala ya jamii wameitaka Idara ya Mahakama nchini kuwapa adhabu kali wanaotekeleza ubakaji na dhulma za kijnsia kwa watoto wa kike na wanawake na kuwalinda.

Akiongea na wanahabari huko Likoni mjini Mombasa siku ya Jumamosi, mwanaharakati wa kundi la Sauti ya Wanawake Pwani Amina Juma alisema kwamba visa vya ubakaji kwa watoto wa kike vimekithiri mno katika maeneo la Likoni, Kisauni na Jomvu.

Amina amemtaka Jaji mkuu Dkt Willy Mutunga kuidhinisha kifungo cha maisha gerezani sambamba na kesi zao kuchukua muda mfupi kwa watakaopatikana wakitekeleza uovu huo, kwani visa hivyo vinawaathiri sana watoto wa kike na wanawake.

“Tunaitaka serikali, kupitia jaji mkuu kuidhinisha serikali kwa wabakaji na ikiwezekana kuwafunga gerezani maisha ili kuwa funzo kwa wanaowanyanyasa watoto wa kike na wanawake,” alieleza Amina.

Mapendekezo ya kundi hilo yamejiri baada ya kushuhudiwa visa vya ubakaji na kisha kuuwawa kwa watoto na wanawake na wahalifu hao.