Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mahakama ya Nakuru Jumatano iliskiza Kesi ambapo Robert Mungai ameshtakiwa kwa kosa la kusambaza jumbe za mashambulizi ya kigaidi.

Mungai, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu alitiwa mbaroni mnamo mwezi Aprili, 2015 kwa madai ya kusambaza jumbe hizo kwenye mtandao wa chuo hicho na hivyo kuzua hofu.

Mbele ya Jaji Liz Gicheha, upande wa mashtaka ulitoa ushahidi wake kumhusisha mshukiwa na kosa hilo.

Afisa wa uchunguzi alitoa stakabadhi walizopata kwenye mtandao wa Facebook wa Mungai na kusema kuwa ujumbe huo ulikuwa umeandikwa na mshukiwa.

Mashahidi zaidi wanatarajiwa kutoa ushahidi wao kwenye kesi hiyo Februari 10, 2016.

Mshukiwa atasalia korokoroni baada ya kushindwa kutoa bondi ya shilingi 750, 000.