Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Makahaba wanaofanya biashara yao mjini Nakuru wameonywa dhidi ya kuendesha shughuli zao mchana.

Kamanda wa polisi mjini Nakuru Hassan Barua amesema kuwa shuguli za biashara ya ngono zimeongezeka sana mjini Nakuru haswa nyakati za mchana.

Akiongea na wanahabari afisini mwake alhamisi jioni,Barua alisema kuwa polisi hawataruhusu makahaba kuendesha biashara ilioharamishwa iwe mchana ama usiku.

“Kuna mambo ambayo yanafanyika hapa mchana ambayo si mazuri na sisi hatutaruhusu yaendelee. Hao makahaba wameonywa dhidi ya kuendehsa shuguli zao mchana katika baadhi ya barabara za mji na wasipokoma basi tutalazimika kuwaodnoa kwa nguvu na kuwashtaki mahakamani,” alisema Barua.

Aidha Barua allitaka serikali ya kaunti ktuoa ilani ya kufungwa kwa baa na majumba yote yanayotumika kama madanguro nyakati za mchana.

“Kuna baadhi ya nyumba ambazo zinatumika kufanya biashara hiyo mchana na serikali ya kaunti ina jukumu la kufunga majumba hayo ili kukomesha biashara hii,” akasema

Alionya kuwa makahaba watakaopatikana wakiendesha biashara hiyo watakamatwa pamoja na wateja wao.

“Tukiwapata tutawashika na hao wanaume na wote watakwenda mahakamani na wenye hizo nyumba pia tutawashtaki,’’ aliongeza.

Mkuu huyo wa polisi aliwataka wazazi walio na watoto wa kike kuwachunga kwa karibu watoto wao msimu huu wa krismasi ili wasije wakashawishiwa kujiunga na biashara ya ngono na unywaji wa pombe.