Mshukiwa wa mauaji ya mwanamziki Diana Chemuta Chelele alifikishwa kwenye mahakama ya juu Naivasha na kukanusha madai ya mauaji.
Mshtakiwa Erick Makau alikanusha mashtaka hayo mbele ya jaji wa mahakama ya Naivasha Christine Meoli.
Makau alikuwa na uhusiano na mwanamziki huyo huku ikidaiwa kuwa ndoa yao ilikuwa na misukosuko na huenda mzozo wa kimapenzi ulizuka.
Familia za mwendazake pia waliteta kuhusu kuhamishwa kwa kesi hiyo kutoka mahakama kuu ya Kericho.
Kesi hiyo itaskizwa Mei 19.