Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali imetakiwa ikabiliane vikali na makundi haramu nchini sawa na vile serikali inavyokabiliana na kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Mbunge wa Nakuru Magharibi Samuel Arama alisema ni makaso kwa vikundi haramu vinavyochipuza pamoja na vile ambavyo vimekuwa vikiwahangaisha wakaazi kimyakimya katika maeneo mbalimbali nchini vinafaa vikabiliwe kwa mujibu wa sheria.

Aliongeza kwamba lengo la vikundi hivyo ni aidha kufanya mauaji au hata kuleta hali ya wasiwasi miongmi mwa wakaazi.

Arama aidha amesema kuwa ni wajibu wa serikali kuhakikisha wakenya wanalindwa dhidi ya mashambulizi yoyote na kuhakikisha usalama na mali ya wakenya inalindwa kikamilifu.

Kutokana na madai ya kusambazwa kwa vijikaratasi na kundi moja haramu hapa mjini Nakuru, mbunge huyo alisisitizia maafisaa wa polisi wapige jeki doria za polisi na kuhakikisha hakuna taharuki yoyote kwa ajili ya maendeleo.

Haya yanajiri baada ya wafanyabiashara wawili kuuwa hali ambayo ilipelekea wasiwasi Nakuru.