Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mazingira mabaya ya jinsi mtoto analelewa kimetajwa kuwa chanzo kikuu cha baadhi ya vijana kujipata katika athari ya kujiingiza katika itikadi kali na maswala ya ugaidi na uhalifu kwa jumla.

Kwenye hotuba iliyotolewa katika hafla inayoendelea katika ukumbi wa Free Town katika eneo bunge la Kisauni jijini Mombasa siku ya Jumanne, mkurugenzi wa shirika la Kenya Community Secure Centre, Pyllis Muema alisema kuwa vijana wengi wanajipata katika masuala ya ugaidi kwa sababu mahali wanakulia na mazingira wanamolelewa kuwa ya uhalifu.

Aliongeza kuwa mara nyingi mtoto akikulia kwenye mazingira yaliyo na historia ya uhalifu na ushawishi wa kihalifu, ni rahisi vijana wengine kuweza kuvutiwa na matendo ya wenzao, na kusema ni juhudi za kila mmoja kwenye jamii kwa ushirikiano na mashirika ya jamii kusawisha hali kwa kuwajumuisha vijana kwenye masuala ambayo yatawafaa vyema.

Muema alisema kuwa shirika lake limejitolea kuona kuwa majanga na changamoto za itikadi pamoja na masuala mengine yanayowaathiri vijana kutoka kaunti hiyo na eneo la Pwani kwa jumla yanapata suluhu na kujaribu kuwaleta vijana karibu na miradi ambayo itawafaidi kwenye maisha yao ya usoni.

Mkutano huo ambao ulianza siku ya Jumatatu umeshuhudia vijana wengi kutoka mitaa mbali mbali ya kaunti wakihudhuria, ambapo msomi maarufu na mwanaharakati wa masuala ya jamii Dkt Othman Mujahid kutoka chuo kikuu cha Pwani alikuwa mgeni alikwa.