Mwanamke mmoja ambaye alikiri kosa la kupatikana na pombe haramu aina ya chang’aa alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani na mahakama ya Nakuru.
Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa kupatikana na lita mia moja za pombe hiyo haramu bila leseni katika shamba la Ndusu mjini Njoro.
Ni shtaka ambalo alikiri mbele ya hakimu Liz Gicheha na kuomba mahakama hiyo kumsamehe.
Hata hivyo, alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani ama faini ya shilingi elfu mia moja pesa taslim.
Aidha, amehukumiwa kifungo cha na miezi kumi na moja ama faini ya shilingi elfu hamsini pesa taslim kwenye kosa la pili la kuuza pombe hiyo bila leseni.