Mwanamke mmoja wa umri wa makamu alijeruhiwa vibaya hiyo jana, Jumapili baada ya ya kuteleza na kuanguka kutoka kwa boda boda huko Kiratina.
Mwanamke huyo ambaye inasemekana alikua ameabiri bodaboda hiyo kumpeleka kanisani eneo la Free Area alianguka kutoka boda boda hiyo wakati mhudumu mwendeshaji alipogonga tuta kwenye barabara.
Kulingana na aliyeshuhudia ajali hiyo Robert Maina, mwanamke huyo alipata majeraha ya miguu na mikono, baadaye alikimbizwa kwenye hospitali moja ya kibinafsi (Rafa Medical Clinic) kufanyiwa huduma ya kwanza na baadaye akapelekwa hospitalini.
"Huyu mwanadada ameanguka kutoka kwenye bodaboda wakati mhudumu alipogonga tuta akiwa kwenye mwendo wa kasi. Ameumia miguu na mikono," alisema Maina.
Mhudumu wa bodaboda hiyo ambaye aliepuka bila majeraha alikua miongoni mwa wale walio msaidia mama huyo.