Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Idara ya usalama kaunti ya Mombasa inapata changamoto kuwatia mbaroni walanguzi wakuu wa mihadharati baada ya kukosekana ushahidi wakutosha dhidi yao.

Akizungumza kwenye kikao na wanahabari afisini mwake siku ya Jumanne, Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa alisema kuwa kufikia sasa, walanguzi hawajakamatwa licha ya idara hiyo kujizatiti kuwatafuta.

"Hawa walanguzi wakuu wanatuangaisha kuwatia mbaroni kwa sababu hatuna ushahidi wa kutosha kuwahusisha na ulanguzi huo, tunaomba wananchi washirikianae na polisi katika kuwafichua walanguzi ili wakabiliwe kisheria," alisema Marwa.

Aidha, aliongeza kuwa maafisa wa polisi wamefanikiwa kuwatia mbaroni watumizi 668 wa dawa za kulevya na kufanikiwa kufunga maskani 86 ya watumizi wa midharati.

Marwa aliwataka wananchi kushirikiana na polisi katika kutoa taarifa kuhusu walanguzi hao ili hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Wakati huo huo, aliongeza kuwa usalama umeimarika jijini baada ya vijana wanaotumia mihadharati kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka na wengine kufungwa katika gereza la shimo la Tewa.