Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa ameteuliwa kuwa mratibu wa ukanda wa Pwani na atachukua nafasi ya Samuel Kilele ambaye amehamishwa hadi eneo la Magharibi mwa Kenya.

Katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa na waziri wa usalama wa ndani na uratibu wa taifa Joseph Nkasseirry, aliyekuwa mratibu wa eneo la Magharibi mwa Kenya James Ole Serian amehamishwa hadi jijini Nairobi.

Eneo la bonde la ufa limegawanya katika maeneo mawili, eneo la kusini mwa Mombasa litakalongozwa na Wanyama Musiambo makao yake makuu yakiwa mjini Nakuru huku Kaskazini mwa Bonde la Ufa kutaongozwa na aliyekuwa katibu katika wizara ya usalama Joseph Irungu.

Aidha Claire Omollo, aliyekuwa mratibu wa mashariki mwa Kenya, Osman Warfa aliyekuwa akihudumu Bonde la Ufa, Njoroge Ndirangu wa Nairobi na Francis Mutie wa Nyanza wamehamishwa hadi jumba la Harambee jijini Nairobi.

Hatua hiyo ya kugawanya eneo la Bonde la Ufa inalenga kuboresha oparsheni za kiusalama katika eneo hilo baada ya kushuhudia changamoto haswa za vita vya kiukoo zinazosababishwa na masuala ya ardhi.

Mabadiliko haya yanakuja kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao ambapo utawala wa mikoa ulifanyiwa mageuzi na kutowaondoa madarakani wakuu wa mikoa ambao kwa kwa sasa ni waratibu wa taifa katika maeneo hayo baada ya kupitishwa katiba mpya mwaka 2010.