Wapenzi wa muziki katika kaunti ya Nakuru na nchini wanaomboleza kifo cha mwanamuziki Paul Mwangi almaarufu Salim Junior.
Salim Junior ambaye amatoka katika eneo bunge la Subukia aliaga dunia katika hospitali ya War Memorial .
Kupitia kwa mahojiano kwa njia ya simu Jumamosi, wanamuziki wa Nakuru miongoni mwao Simon Ben, Muraya wa Tutu, Slim wa Muthoni, General wa Mathina, Saida wa Mugure na Njoroge wa Njoki wametaja kifo cha marehemu kama pigo kubwa kwa sekta ya muziki huku akisema alikuwa kigezo chema cha kuigwa na wengine haswaa katika eneo la Subukia.
Inaarifiwa kuwa ndugu na dada za marehemu wanaofahamika kama Mighty Salim, Salim Young na Sarafina Salim pia ni wanamuziki waliofuata nyayo katika uimbaji.
Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri amesema marehemu Salim Juniour alikuwa na maono mema kwa wale ambao wanaingia katika sekta ya muziki katika kaunti ya Nakuru akisema kwamba alikuwa na mpango wa kuanzisha shule kukuza talanta katika eneo bunge la Bahati.