Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Zaidi ya mashirika 50 yasiyokuwa ya serikali yameungana kushirikiana na Idara ya Vijana eneo la Pwani katika juhudi za kuwaendeleza vijana kiuchumi.

Akizungumza na wanahabari baada ya kuhudhuria kongamano la vijana katika hoteli moja mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Mkurugenzi wa Idara hiyo Mwangome Shumaa, alisema idara hiyo itahakikisha kwamba miradi mwafaka inaidhinishwa ili kuwakuza vijana kibiashara na kuimarisha uchumi.

Kulingana na Bw Shumaa, vijana wengi hujihusisha na uhalifu kutokana na kukosa ushauri mwafaka na mwelekeo wa kujihusisha na ubunifu wa miradi itakayowawezesha kukimu mahitaji hao, hivyo basi lazima swala hilo kuidhinisha.

“Tumejitokeza kuwaunganisha vijana katika ubunifu wa miradi mbalimbali ili kuona kwamba tunawasaidia vijana na biashara ndogo ndogo na kuinua uchumi wao ndiposa tumeungana na mashirika ya kijamii," alisema Bw Shumaa.

Bw Shumaa aidha alieleza kuwa muungano huo unawaangazia zaidi vijana katika masuala ya biashara na miradi.