Mshirikishi wa baraza la kitafa la wanawake nchini Amina Raidhwan amesema kuwa ni jukumu la kina mama kujitokeza na kuwania nyadhifa mbali mbali serikalini katika uchaguzi mkuu ujao.
Akiongea katika sherehe ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani siku ya Jumanne katika eneo la Likoni, Kaunti ya Mombasa, Raidhwan alisema kuwa kina mama wanapaswa kuhamasishwa ili kujua haki zao za kikatiba na majukumu yao kama viongozi wa kike.
Wanawake shujaa 20, wakiwemo Mekatilili Wa Menza aliyepigania uhuru wa taifa hili, Margaret Kenyatta, Wangare Mathaai, Agnes Mawondo ambaye ni mwanamke wa kwanza kupata shahada Afrika ya Mashariki, waliweza kutuzwa vyeti mbali mbali kutokana na mchango wao katika ujenzi wa taifa.