Share news tips with us here at Hivisasa

Waziri wa elimu nchini Dkt Fred Matiang’i amepongezwa kwa kuongezea chuo kikuu cha Kisii muda wa miezi 12 kuafikia mahitaji yanayostahili kielimu kabla ya mabewa yake kufungwa.

Hii ni baada ya waziri huyo kuandaa kikao na tume inayosimamia vyuo vikuu nchini na washikadau wa elimu na kukubaliana kuongezea chuo hicho muda zaidi kuafikia yale yanahitajika kielimu.

Wakizungmza na mwandishi huyu mnamo siku ya Jumatano mjini Kisii, idadi kubwa ya wazazi walimpongeza Matiang’i kwa juhudi za kuhakikisha wanao hawaathiriki kimasomo kwani wengi wao walikuwa tayari wamelipa karo na wengine wako karibu kumaliza masomo yao.

“Uamuzi wa waziri Matiang’i ni wa kufurahisha na huo ndio uongozi tunahitaji nchini, na tunampongeza kwa kutimiza ahadi aliyoitoa kwetu kuwa jambo hilo angelishughulikia na amefanya hivyo,” alisema James Makori, mzazi mmoja.

Aidha, naibu gavana wa Kaunti ya Kisii Joash Maangi naye pia alipokea uamuzi wa waziri Matiang’i kwa kuongezea chuo hicho kikuu muda kujipanga na kuafikia yale yanahitajika kimasomo

Wiki moja iliyopita, tume inayosimamia vyuo vikuu nchini ilidai kufunga mabewa 10 ya chuo kikuu cha Kisii kufuatia kutoafikia mahitaji ya kielimu.