Leo itakuwa siku kuu kote nchini kwa zaidi ya watahiniwa nusu milioni waliofanya mtihani wao wa kidato cha nne mwaka jana, huku wakisubiri matokeo ya mtihani yao.
Waziri wa Elimu Fred Matiang’i anatazamiwa kutangaza matokeo hayo hii leo jijini Nairobi na watahiniwa wa mwaka uliopita watapata matokeo yao kwa njia ya simu kupitia nambari 22252 au kwenye tovuti ya KNEC, pindi tu waziri atakapokamilisha kutangaza matokeo hayo.
Mtihani ya kidato cha nne wa mwaka 2015 ulikumbwa na matatizo mengi yanayotishia uaminifu wa matokeo ya mtihani huo na KNEC wanatarajiwa kubadili utendakazi wao ili kupambana na tatizo hilo hasa ikizingatiwa kuwa kumeibuka hali ya wasiwasi miongoni mwa wadau katika sekta ya elimu nchini.
Inadaiwa kuwa idadi kubwa ya shule zilizotajwa kwenye madai hayo ni shule maarufu nchini, hasa zilizoko katika eneo la Nyanza na kuwa wadau katika sekta hiyo wanaitaka baraza la mitihani KNEC kutoa maelezo kuhusiana na madai hayo kabla ya tutangaza rasmi matokeo.