Share news tips with us here at Hivisasa

Matumizi ya mbolea ya kisasa katika upanzi na ukuzaji wa vyakula huenda ukawa na athari kubwa sana za kiafya katika mwili wa binadamu, mtaalamu wa afya amesema.

Kulingana na Damaris Kisika ambaye ni mtaalamu wa afya na lishe bora, mbolea ya kisasa inayotumiwa katika kukuza vyakula ina kemikali ambazo hujikusanya katika vyakula hivyo na baadayae kujitokeza na kuwa na athari mwilinivyakula hivyo vinapokuliwa.

Akiongea katika shule ya msingi ya kiamaina wakati wa hamasisho kuhusu umuhimu wa kutumia mbolea ya kienyeji,Kisika alisema kuwa kemikali hizo ndizo huchangia katika kusababisha magonjwa kama vile saratani katika mwili wa binadamu.

“Hizi mbolea za kisasa ni kemikali tupu na mmea unapokula kemikali hizo na baadayae utoe zao litakalo liwa na binadamu basi huyo binadamu ataathirika kutokana na kemikali hizo,” alisema Kisika.

“Wingi wa magonjwa na maradhi ya kisasa tunayoshuhudia yanatokana na wingi wa kemikali katika vyakula vyetu an hizi kemikali zinatokana na mbolea na madawa mengine ya kilimo,” aliongeza.

Mwenyekiti wa Kiamaina organic farmers Daniel Mwangi aliwataka wakulima kutotegemea mbolea za kisasa katika upanzi na badala yake kutumia mbolea ya kujitengenezea nyumbani.

“Hii mbolea ya kisasa ina sumu inayochoma mchanga na kuudhoofisha baada ya kutumiwa kwa muda mrefu na iwapo tutatumia mbolea ya kienyeji kwa wingi basi tutatunza mashamba yetu na pia kupunguza athari za kiafya kwa mifugo na hata binadamu wanaotumia mazao kutoka mashamba yetu,” alisema Mwangi.