Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Watoto mayatima wanaoishi kwenye makao ya Risa wamepata sababu ya kutabasamu krismasi hii baada yakupokea ufadhili wa vyakula, nguo, viatu na malazi kutoka kwa kundi moja la vijana.

Akihutubu siku ya Jumatano kwenye makao hayo ya watoto, kiongozi wa kundi hilo Beavon Magare, alisema kuwa watoto wengi mayatima huwa na ugumu kupata elimu kutokana na kutopata ufadhili kutoka kwa wanajamii.

"Malezi ya watoto ni jukumu la jamii na wala sio la mtu mmoja na kama jamii, sharti tuungane ili kuhakikisha kuwa mayatima wanapata haki zao hasa kwa kuwafadhili kupata elimu," alisema Magare.

Magare aidha aliipa changamoto serikali ya kaunti ya Nyamira na viongozi wa kisiasa kutafuta mbinu zakuhakikisha kuwa mayatima wanapata ufadhili wa kimasomo ili kuwasaidia kusoma hadi vyuo vikuu.

"Tunalo stahili kujua ni kuwa huenda wasimamizi wa makao ya mayatima wasiwe na uwezo wa kuwafadhili mayatima kwa njia zote na ndio maana ninapendekeza kwamba serikali ya kaunti hii kwa ushirikiano na viongozi wa kisiasa, watafute njia ya kufadhili masomo ya mayatima hawa ili waweze kupata elimu itakayo wafaa siku za usoni," alisema Magare.