Share news tips with us here at Hivisasa

Viongozi wa mrengo wa Cord wameupinga mradi wa huduma kwa vijana ulioanzishwa katika eneo la Malindi.

Wakiongozwa na mwakilishi wa wanawake katika Kaunti ya Mombasa Mishi Mboko, viongozi hao walidai kuwa mradi huo ni njama ya Jubilee kujipigia debe kisiasa kwenye uchaguzi mdogo wa eneo hilo.

Aidha, Mboko alisisitiza kuwa serikali ingeshughulikia swala la mamilioni ya pesa za NYS zilizopotea badala ya kuzindua miradi hiyo ovyo ovyo.

Mboko aliyasema haya siku ya Alhamisi, alipokuwa akihutubia wananchi wa seheumu hiyo, huku akiwasihi kumpigia kura kiongozi wa ODM.

Aliongeza kuwa kuchaguliwa kwa mbunge wa ODM katika sehemu hiyo itakuwa bora kwani kutaongeza idadi ya wabunge pinzani katika bunge la kitaifa.