Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua ameomba makanisa mbalimbali katika kaunti hiyo kuungana pamoja na kusimama imara ili kupigana na vita dhidi ya ukabila ambayo imekuwa pigo kubwa katika maendeleo nchini.

Mbugua, akizungumza siku ya Jumapili katika kanisa la Victors Chapel jijini Naivasha pia aliahidi kusaidia kanisa hilo na makanisa mengineyo kufuatia juhudi zao za kuleta amani katika kaunti hiyo.

"Sisi sote tuko sawa mbele ya mwenyezi Mungu, hivyo basi hakuna haja ya kutengana kwa msingi wa kikabila. Hii ndiyo maana kaunti hii iko imara kusaidiana na kanisa hili na makanisa mengine ambayo yanalenga kudumisha amani na umoja katika eneo hili," Mbugua alielezea.

Gavana huyo pia alielezea imani yake kwa makanisa katika kumaliza ukabila nchini akielezea kuwa ni kanisa ambapo watu kutoka sehemu mbalimbali nchini hutangamana na kuomba pamoja.

Kanisa hilo lilikuwa likiadhimisha miaka kumi tangu kuzinduliwa kwake.