Share news tips with us here at Hivisasa

Shirika la Lions Club lililoko jijini Nakuru limekabidhi kaunti ya Nakuru bidhaa yanye dhamana ya shilingi 250,000 za kuwasaidia watu na familia zisizojiweza. Shirika hilo lilimkabidhia gavana wa kaunti hiyo Kinuthia Mbugua biadhaa hizo ambazo zitapewa watu maskini katika maeneo mbalimbali kutoka kaunti hiyo.

Mbugua akipokea bidhaa hizo siku ya Jumamosi jijini Nakuru alishukuru shirika hilo kwa juhudi walizoonyesha kusaidia watu maskini huku akiahidi kuungana nao kuimarisha maisha ya wananchi wa kaunti hiyo.

"Ni jambo la kufurahisha kuona shirika hili limejitolea kusaidia watu wasiojiweza na bidhaa hizi. Kwangu ni kuwashukuru na kuahidi kuwasaidia kwa namna yoyote ile kama kaunti," Mbugua alisema.

Mbugua pia alikubali ombi la shirika hilo la kutaka kuboreshwa kwa barabara inayoelekea kwa wafadhili wa shirika hilo.

"Misaada ambayo tumeweza kupata kutoka kwa shirika hili ni nyingi na haiwezi linganishwa na ombi lenye la kutaka kuboreshwa kwa barabara hiyo. Kama serikali ya kaunti tutahakikisha jambo hilo linashughulikiwa haraka iwezekanavyo," Mbugua aliongezSa.

Rais washirika hilo Yashvi Shah pia aliahidi kushirikiana na shirika la Kinuthia Mbugua Foundation ili kuhakikisha kaunti hiyo inaendelea na wanachi wanapata kufurahia.