Share news tips with us here at Hivisasa

Vijana wametakiwa kuendelea kusajili kampuni na baadaye kutafuta kandarasi kwenye serikali ya kaunti ya Nakuru kwa minajili ya kujiendeleza.

Wito huu umetolewa na gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua.

Akizungumza kwenye eneo la Berur Rongai mnamo Ijumaa Kinuthia alisema kwamba, aslimia 30 ya kandarasi kwenye serikali ya kaunti zimetengewa vijana na akina mama.

Alisema: “Kandarasi hizi zitasaidia kupigana na ukosefu wa ajira miongoni mwenu vijana na akina mama kwa sababu umaskini umekidhiri kaunti ya Nakuru.”

Wakati uo huo Kinuthia aliwataka viongozi wa Rongai kuendelea kushirikiana na serikali yake kwa ajili ya kuwapelekea wananchi maendeleo mashinani.