Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua amewamiminia sifa wananchi wa kaunti hiyo kwa kusimama naye katika uongozi wake na kuwa watulivu huku serikali hiyo ikiendelea na kutoa huduma kwa wakaazi wa eneo hilo.
Mbugua alikuwa akizungumza siku ya Jumatano katika eneo la Kampi Ya Moto Center, kaunti ndogo ya Rongai ambako ameendeleza mradi wake wa Gavana Mtaani unaoingia mkondo wake wa tano. Mbugua pia amehakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa serikali yake itakuwa imara kuhakikisha eneo hilo linapata kuendelea.
‘Ni nyinyi wananchi ndio mlituajiri na hivyo baso hatuna budi ila kuwatumikia. Ndiyo maana tumefika eneo hili ili tuwasaidie kwa namna yoyote ile. Lengo la mradi huu wa Gavana Mtaani ni kuleta huduma za seikali ya kunti karibu na wananchi ili mpate kunufaika.’ Mbugua alielezea.Gavana huyo ambaye pia aliambatana na wakuu wengine katika serikali yake akiwemo naibu wake Joseph Ruto anatarajiwa kuongoza shughuli hiyo kwa siku mbili kabla ya kuelekea eneo la Subukia tarehe 16 na 17 baadaye mwezi huu.