Gavana wa jimbo la Nakuru Kinuthia Mbugua amezitaka kanisa na viongozi wote wa kidini katika kaunti kushirikiana na serikali yake katika kusitisha mivinyo ya kizazi kipya aliyodai imeanza kurejelea swala ambalo anadai linarejesha nyuma jitihada zilizoafikiwa katika amri ya Rais Uhuru Kenyatta.
Akiongea mjini Nakuru Jumanne, Mbugua amesema kuwa swala la unywaji wa pombe linahitaji matibabu rasmi na hata viongozi wa kidini kuingilia kati akitaja haja ya kuhusisha kanisa kwa vikao vya kuuhamasisha umma.
Wakati uo huo Mbugua ameipa kamati ya kuthibiti vileo katika jimbo ndogo la Naivasha wiki moja kufunga vituo vyote pamoja na kuwatia mbaroni wahusika katika biashara hiyo haramu haswa katika eneo la Karagita alilosema linasalia nyuma kutokanana uhalifu wa aina hiyo.
“Serikali yangu haitakaa na kushuhudia biashara hii amayo zimewaangamiza vijana wengi kuendelezwa katika kaunti hii nitafanya kila jitihada kuimarisha hali ya maisha ya kila mkaazi wa kaunti hii," alisema Mbugua.
Hata hivyo amesema kuwa seriklai yake imetimiza aslimia 75 ya ahadi zake kwa mwananchi akitaja vijana kuwa wengi wa walionufaika huku akiahidi kutimiza kulikosalia kwa kipindi kifupi kijacho.