Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua, amewataka wakaazi katika jimbo hilo kufahamu umuhimu wa kuwa na kadi ya kupiga kura.

Kinuthia akihutubia wakaazi kwenye barabara ya Kenyatta Avenue katikati ya mji wa Nakuru Jumanne, alisema kila baada ya miaka mitano, mwananchi yeyote yule, huwa na usemi katika kuamua ni nani atamwongoza katika kipindi kingine cha miaka mitano.

“Kura hufanya sisi wote sawa, kwa kusawazisha kila mwananchi, hakuna tajiri au maskini, ama kura yenye uzito kuliko nyingine,” alisema Mbugua.

Gavana huyo aliwataka Wakenya haswa wakaazi wa jimbo lake kutumia fursa ya siku 30 iliyotolewa na tume ya uchaguzi nchini IEBC kujiandikisha kama wapiga kura.

“Ningetaka kuwahimiza wazazi, makanisa, shule na taasisi zingine, waweze kuhimiza vijana wajue umuhimu wa kuwa na kadi ya kupiga kura, na kwenda kujiandikisha ili wawe waamuzi wazuri wa maisha yao ya baadaye kuhusu uongozi wa taifa.”