Mbunge wa Mvita Abdulswammad Nassir ameghadhabishwa kuhusiana na idadi ndogo ya wananchi wanaojitokeza katika zoezi la kusajili wapiga kura eneo la Mombasa.
Akizungumza katika wadi ya Mji wa Kale siku ya Jumatatu, Nassir alisema kuwa jambo hilo ni la kusikitisha kuona kuwa wananchi wanajikokota katika kujiandikisha kama wapiga kura.
Amedokeza kuwa kufikia sasa ni wakaazi 719 kutoka eneo bunge hilo waliojisajili kama wapiga kura tangu kuanzishwa kwa zoezi hilo wiki iliyopita, huku wadi ya Mji wa Kale ikiandikisha watu 170 pekee.
Aidha, amewataka wananchi wa Mombasa kuhakikisha wanajiandikisha kwa wingi kama wapiga kura ili mageuzi ya haraka ya uongozi bora kupatikana nchini.