Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakazi wa eneo la Kibarani wanalalamikia kuadhrika na vumbi linalotokana na kemikali ya klinka kutoka kwa kiwanda kimoja kilicho karibu na makazi yao.

Wakazi hao walisema kuwa idadi kubwa ya watu wagonjwa katika eneo hilo inatokana na madini hayo ya Klinka.

Wakazi hao walimueleza mwanahabari huyu siku ya Jumatatu kuwa watoto wengi wameadhirika huku wengine ata wakifariki kutokana na madini hayo, huku wakidai kuwa kisa cha hivi majuzi ni kushudiwa vifo vya watoto wanne katika sehemu hiyo.

Mbunge wa Jomvu Badi Twalib alisema watachukua hatua za kisheria dhidi ya kiwanda hicho, huku mbunge huyo akitishia kuwaongoza wakazi hao katika maandamano iwapo kiwanda hicho hakitafungwa kwani kinadhofisha afya ya wakazi wa Jomvu.