Mbunge wa eneo bunge la Borabu Ben Momanyi amewataka viongozi wa kisiasa katika eneo la gusii kuungana pamoja ili kutafuta mwafaka wa mzozo wakimpaka wa Keroka baina ya serikali ya kaunti ya Kisii na ile ya Nyamira.
Akihutubu kwenye hafla ya mazishi kule Keroka siku ya Jumanne, Momanyi alisema kuwa mazungumzo baina ya magavana hao wawili na wabunge wa eneo hilo la mpaka yatasaidia katika kuafikia mwafaka wa mzozo huo.
"Nawaomba wakazi wa hapa Keroka kuendelea kuwa watulivu kwa maana mzozo uliopo haustahili kututenganisha kwa kuwa sisi sote ni watu wa jamii moja na ndio maana sharti viongozi wakisiasa waketi nakutafuta suluhu la mzozo huu kwa haraka," Alisema Momanyi.
Kwa upande wake, mbunge wa Nyaribari Masaba Elijah Moindi alisema kuwa huenda vurugu zinazoshuhudiwa katika eneo hilo zikawa ni zakuchochewa kisiasa.