Share news tips with us here at Hivisasa

Wizara ya maji ya kitaifa imelaumiwa kutokana na uhaba wa maji unaoikumba mkoa wa Pwani.

Lawama hizi zilitolewa na mbunge wa Mvita Abdulswammad Nassir ambaye alisema kuwa waziri wa maji na unyunyizaji Eugene Wamalwa pamoja na serikali ya kitaifa ni ya kulaumiwa kutokana na shida ya uhaba wa maji inayoshuhudiwa eneo la Pwani.

Nassir alidai kuwa kukatwa kwa huduma hiyo muhimu ni njama ya serikali ya Jubilee kujipigia debe kutumia suala hilo linaloaminika kuwa ngome ya muungano wa Cord ili rais aweze kuingilia kati na kupata umaarufu.

Aidha, alisema kuwa deni la shilingi milioni mia sita linalodaiwa serikali ya kaunti ya Mombasa na bodi ya usambazaji maji eneo la Pwani limerithiwa kutoka kwa baraza la Manispaa ya Mombasa, hivyo basi sharti serikali iweze kuwajibika kulipa deni hilo.

Kwa wiki sasa wakazi wa maeneo mbali mbali ya ukanda wa Pwani wanakabiliwa na uhaba wa maji, hali inayolazimu kutumia maji ya kisima huku wengine wakililamikia kukwama kwa shughuli zao.

Mbunge huyo alikuwa akizungumza siku ya Jumatano wakati wa ziara pamoja na Raila Odinga.