Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuingilia swala la maafisa wa polisi kuwashika watu ovyo ovyo hasa nyakati za usiku.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa mwangaza mitaani siku ya Ijumaa katika uwanja wa Makadara Jijini Mombasa, mbunge huyo alilalamika kuhusu maafisa wa polisi kuwadhulumu wakazi, haswa vijana nyakati za usiku.
Abdulswamad alimueleza rais kuwa inakuwa vigumu kwa watu kutoka usiku kwa kuhofia kukamatwa na misako ya mara kwa mara inayofanywa.
Abdulswamad alisema kuwa misako hiyo inafanywa kwa njia isiyokuwa ya kitaalamu, hivyo kusababisha kushikwa kwa wingi watu wasiokuwa na hatia.
Kauli yake inajiri baada ya kushudiwa visa vya maafisa wa polisi kuwashikia na kuwaangaisha wananchi wa eneo bunge lake.