Mbunge wa Mvita Abdulswammad Shariff Nassir ametishia kuwataja maafisa wa polisi wanaowanyanyasa wakazi wa eneo bunge lake iwapo hawatakoma.
Nassir alisema siku ya Ijumaa katika eneo bunge lake kuwa wakazi wa eneo bunge hilo wanakosa amani pindi tu kunapokuwa na misako ambayo lengo kuu ni kuwadhulumu raia wala si kutafuta magadi.
Aidha, aliwalaani polisi kwa kuwasishika vijana wasiokuwa na hatia na kuwasingizia kuwa ni magadi.
Nassir aliwataka polisi kubadilisha mbinu za kukabiliana na magaidi ipasavyo wala si kuwakandamiza wananchi kunapotokea uahilifu.
“Nitawataja polisi ambao kazi yao ni kuwadhulumu raia kwa visingizio eti wanatafuta wahalifu iwapo hawatakoma,” alisema Abdulswammad.
Haya yanajiri baada ya kushuhudiwa idadi kubwa ya wananchi katika eneo hilo wanaodai kunyanyaswa na maafisa wa polisi pasi sababu mwafaka.