Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir amezindua rasmi mradi wa chakula kwa watahiniwa wote wa darasa la nane kutoka eneo bunge lake.

Akizindua mradi huo siku ya Jumanne katika shule ya msingi ya Makande, Nassir alitoa wito kwa watahiniwa hao kutia bidii katika mtihani huo kwani ni mhimu sana kwa maisha yao ya usoni.

Aidha, mbunge huyo aliahidi kufadhili wanafunzi watatu bora wa kidato cha nne na wale wa darasa la nane kutoka kila shule ya eneo bunge hilo iwapo watafaulu vyema.

Mradi huo wa chakula cha mchana kwa watahiniwa ulianzishwa rasmi miaka sita iliyopita na wakfu wa Shariff Nassir chini ya usimamizi wa mbunge huyo.

Mtihani huo wa kitaifa ulianza rasmi kote nchini siku ya Jumanne, na kutarajiwa kukamilika siku ya Alhamisi ambapo jumla ya wanafunzi laki tisa wanakalia mtihani huo kote nchini.