Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakulima wanaoendeleza ukulima kando ya mto Rongai wamesababisha uhaba wa maji kwenye wadi ya Sowin Rongai, kulingana na MCA wa wadi hiyo Simon Molok.

Akizungumza na mwandishi huyu, bwana Molok alisema kwamba wananchi wa wadi yake wanalazimika kusafiri kilomita 8 hadi Mogotio ili kutafuta bidhaa hiyo muhimu.

Alisema maji ya kisima cha Lomolo B sio safi kwa matumizi ya kinyumbani, kwani yamebadili rangi na kuwa ya manjano na hivyo watu wanakimbilia maji ya mto huo ambayo pia yameharibiwa na wakulima hao.

Ameutaka utawala wa mkoa kuwachulia wakulima hao hatua kali za kisheria haraka, kwa kukiuka haki za wengine kutumia maji safi.

Hata hivyo alisema ofisi yake na serikali ya kaunti ya Nakuru wanafanya hima kuhakikisha kila Mwananchi anapata maji safi ya matumizi.