Siku kadhaa baada ya mhudumu mmoja wa bodaboda kutekwa nyara na watu wasiyojulikana huko Elburgon,mwakilishi wa wadi hiyo Florence Wambui ameitaka idara ya polisi kuwajibika.

Share news tips with us here at Hivisasa

Katika mahojiano naye kwa njia ya simu,Wambui aliitaka idara ya polisi kuimarisha doria eneo hilo hasa majira ya usiku.

Vile vile ametaka polisi kuhakikisha kwamba waliotenda uovu huo wanapatikana na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

"Ningependa kutoa wito wangu kwa polisi tafadhali,hili swala si la kuchukulia mzaha na sharti aliyehusika atiwe mbaroni na kuchukuliwa hatua kali"alisema Wambui.

Wakati huo huo, MCA Wambui amewataka vijana wa eneo hilo kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea.

Matamshi yake yanajiri hata baada ya wahudumu wa bodaboda kufanya maandamano eneo hilo wakilalamikia kutiwa mbaro kwa mmoja wao.