Meli ya kitalii ya MS Insignia kutoka Zanzibar imetia nanga katika bandari ya Mombasa ikiwa na abiria 607 pamoja na wahudumu wa meli hiyo 400.
Akiongea na wanahabari katika bandari Mombasa siku ya Jumatatu, baada ya kupokea watalii hao, kwa niaba ya kaimu mkurugenzi wa bandari hiyo Catherine Wairi, Afisa wa Mawasiliano katika Halmashauri ya Bandari Mombasa KPA, Hajj Masemo alisema kuwa watalii hao watazuri katika Mbunga mbali mbali za wanyamapori ikiwemo Mwaluganze na maeneo mengi ya kitalii.
Alisema kuwa tayari wasimamizi wa bandari hiyo pamoja na wadau wa sekta ya utalii na Wizara ya utalii chini ya Waziri wa Utalii Najib Balala waliandaa mikakati ya kuuza taifa hili kitalii katika mataifa ya magharibu ikiwemo Ugerumani, Marekani, Ushelisheli na Uingereza.
"Tumeandaa mikakati mwafaka ya kuhakikisha kuwa tunaliuza taifa hili kitalii katika mataifa aya magharibi kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inaimarika ndio maana tumejaandaa kuzuru nchi hizo,"alisema Masmo.
Wakati uo huo alisema kuwa eneo la kuwakaribisha watalii katika bandari hiyo linatayarijiwa kuanza kukarabatiwa mwezi Aprili wakati wa msimu mchache wa watalii kwani tayari shilingi milioni 100 zimetengewa ukarabati huo huku akisema kuwa mikakati ya kujenga jingo jipya umepangwa kujengwa katika eneo la Dongo Kundu.
Meli hiyo ya kitalii inahitimisha meli ya 10 tangu meli za kitalii kuanza safari zake za kuzuru humu nchini baada ya mataifa ya magharibi kuondoa marufuku yake ya kuzuia raia wao kuzuru humu nchini huku meli zengine za kitalii zikitarajiwa kuwasili tena kuanzia mwezi Septemba hadi Disemba.
Hata hivyo zaidi ya watalii 371 kutoka Marekani, 116 kutoka Canada, 16 kutoka Autrialia miongoni mwa wengine huku meli hiyo itakarajiwa kuondoka jioni ya leo kuelekea nchini Ushelisheli katika kisiwa cha Mahe mji wa Victoria.