Meneja wa kampuni ya ulinzi ya kibinafsi ya Guard Force Group amefikishwa mahakani kwa tuhuma za jaribio la mauwaji.
Mahakama ilielezwa siku ya Jumatano kuwa kati ya Oktoba 20, 2015 na Oktoba 26,2015, Debra Joyce Otigo anadaiwa kushirikiana na wahalifu wengine, ambao hawakuwa mahakamani, na kumvamia Polycarp Okumu katika eneo la Beach Road Kisauni wakiwa na lengo la kutaka kumuua.
Otigo alikanusha madai hayo mbele ya hakimu Julius Nang’ea.
“Sikuhusika kamwe kwenye njama hiyo na sijui kamwe kisa kama hicho kama kilipangwa, sina habari yeyote kamwe,” alisema Otigo.
Mshukiwa atasalia rumande hadi Novemba 11,2015 kusubiri uamuzi wa kupewa dhamana.