Mfanyibiashara mmoja amefikishwa katika mahakama ya Mombasa kwa kosa la kuingiza makasha nane ya sukari yenye thamani ya shilingi milioni 14 kinyume cha sheria.
Mnamo Oktoba 12, 2016, mshtakiwa huyo kwa jina Amos Gichana Kibagendi pamoja na wenzake ambao hawakuwa mahakamani wanatuhumiwa kuingiza sukari hiyo humu nchini kupitia bandari ya Mombasa.
Mtuhumiwa alikana madai hayo siku ya Jumatano mbele ya hakimu Richard Odenyo na kupewa dhamana ya shilingi milioni 3.
Kesi hiyo itasikilizwa tena Aprili 5,2016.