Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Pasta mmoja anaendelea kuzuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Nyamira baada yake kufumaniwa akishiriki ngono na mwanafunzi wa kidato cha tatu siku ya jumanne jioni. 

Mshukiwa huyo wa unajisi mwenye umri wa miaka alifumaniwa na wananchi akimnajisi mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu nyumbani kwake katika kijiji cha Makairo kwenye wilaya ya Nyamira kusini. 

Kulingana na taarifa za kuaminika ni kuwa msichana muathiriwa alitoka nyumbani kwao akielekea shuleni, na kisha akaamua kupita nyumbani mwa mshukiwa mahali ambapo kitendo hicho kilitokea.

Akithibitisha kisa hicho, OCPD wa Nyamira Ricoh Ngare amesema kuwa ripoti ya uchunguzi wa hospitali kuu ya Nyamira imebaini kuwa msichana huyo ni mja mzito. 

"Ripoti ya uchunguzi ambayo tumeipata kutoka kwenye hospitali kuu ya Nyamira ni kuwa muathiriwa ni mjamzito na ingawaje pasta huyo amekana kumnajisi kwa kudai kuwa alikuwa akimwombea tutangoja mwanafunzi huyo ajifungue kisha vipimo vifanywe kubaini baba ya mtoto ni nani," alisema Ngare.

Ngare ameongeza kwa kusema kuwa wananchi wenye ghadhabu walimpa kichapo mshukiwa huyo wa unajisi baada yao kumpata akitekeleza kitendo hicho kabla yakumuwasilisha kwa maafisa wa polisi. 

"Wananchi wenye ghadhabu walimpa kichapo mshukiwa huyo wa unajisi kabla yakumuwasilisha kwa maafisa wa polisi," alisema Ngare.

Kulingana na wananchi ni kuwa pasta huyo amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi huyo kwa muda mrefu kabla ya siku zake arobaini kutimia.