Mkurugenzi wa bodi ya Nacada katika eneo la Pwani, Sheikh Juma Ngao amesema kuwa ameunga mkono muungano wa Cord kwa kile alichokitaja kama kuhujumiwa na muungano wa Jubilee.
Ngao alisema kuwa Jubilee imeshindwa kuzitekeleza ahadi walizowapa Wapwani wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2013.
Akizungumza siku ya Jumapili, Ngao alisema kuwa Wapwani bado hawajanufaika kimaendeleo licha ya Jubilee kusema kuwa inatoa huduma kwa wananchi wote nchini.
Siku za hivi majuzi kiongozi huyo alionekana kushiriki katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Malindi, huku akimpigia debe mgombea wa chama cha ODM Willy Mtengo.
Hapo awali, Sheikh Ngao alikuwa mfuasi wa mrengo wa Jubilee na ata akachaguliwa tena na Rais Uhuru Kenyatta katika bodi ya Nacada.