Mlinzi wa mheshimiwa amesababisha kizaaza kwa kushtumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi.
Kulitokea kizaazaa nyuma ya hema la waheshimiwa baada ya mlinzi wa kiongozi mmoja wa kisiasa kutoka Uasin-Gishu kushtumiwa kwa madai ya kuwa na tabia ya kuonjaonja mwanafunzi mmoja wa chuo cha kitaifa cha mafunzo anuai cha Eldoret.
Mshikemshike huo ambao ulishuhudiwa kwa dakika chache sana ulitokea pale mzazi wa mwanafunzi husika ambaye pia ni mlinzi wa kibinafsi katika chuo hicho alipomwandama mlinzi husika na kutaka kujua ni kwa nini amekuwa na mazoea ya kuharibia mtoto wake maisha.
“Umekuwa ukionja mtoto wangu kila mara wewe huoni huyu bado ni mwanafunzi nawe unataka kumharibia maisha ni tabia gani hii nitakushtaki kwa mheshimiwa,” alisema mlinzi huyo kwa uchungu.
Matamshi hayo yalionekana kukera mlinzi husika ambaye alimuinukia mwenzake baada ya kupanda mori na kudai kuwa mzee husika alikuwa akimharibia jina bila ushahidi.
“Ushahidi gani unataka na hata ulimtafuna mwanangu Jumatano na nilikuona ni ushahidi gani tena unataka kama hiyo ndio tabia yako mimi sitavumilia uendelee kuharibia mwanangu maisha yake,” aliongeza.
Matamshi hayo yalifanya mlinzi afisa huyo ambaye ni afisa wa polisi wa utawala kuinuka na kuanza kukabana na mlalamishi.
Mlalamishi alinusuriwa na wazee ambao wanafahamiana na afisa huyo ambapo walimuomba atulie huku wakiahidi kutatuta wakati muafaka wa kupatanisha wawili hao na kutafuta suluhu kutokana na uhasama na shtuma hizo.