Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mume na mkewe hii leo, Jumanne wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kumuozesha binti yao mwenye umri wa miaka 14.

Upande wa mashtaka umeeleza mahakama ya mjini Mombasa kuwa mnamo Disemba 24, 2015 katika eneo la Kibokoni, wazazi hao wa mtoto huyo wa miaka 14 wanadaiwa kumuozesha mtoto huyo.

Kulingana na mahakam, hatua hiyo ilitajwa kuwa kinyume na katiba na ukiukaji wa haki za mtoto, huku washtakiwa hao wote wakikanusha madai hayo mbele ya hakimu Richard Odenyo.

Mahakama iliwatoza dhamana ya shilingi laki moja ama pesa taslimu shilingi 50,000.

Kesi hiyo itaskilizwa tena mwezi Machi 22, 2016.